OpenStreetMap logo OpenStreetMap

weeklyOSM 433

Posted by Laura Mugeha on 4 December 2018 in Swahili (Kiswahili).

30.10.2018-05.11.2018

Picha

Kutengeneza Ramani

  • Kwa mujibu wa tweet, Pascal Neis amesasisha ramani yake ya Unmapped Places. Inaelezea makazi mbali na njia kubwa za trafiki. Hata hivyo, makosa ya kutambulisha pia yalipatikana katika nchi zilizotengenezewa ramani vizuri.

  • Stefano Maffulli anapendekeza emergency=fire_alarm_box katika orodha ya barua pepe kwa “kifaa kilichowekwa kwenye ardhi ya umma kutumika kwa taarifa ya idara ya moto ya moto”.

  • Toni Erdmann aliripoti kuhusu zana mpya ya kuthibitisha ubora wa uchambuzi (QA): PTNA (Public Transport Network Analysis) katika orodha ya barua pepe (tafsiri ya moja kwa moja) na katika jukwaa (tafsiri ya moja kwa moja).

  • Makala yenye mada Finding Missing Roads in the Philippines ya Gowin inaelezea kazi yake na njia mpya ya kuthibitisha barabara tovu il kukamilisha barabara nchini Filipino.

  • Zana ya kuthibitisha ubora wa anwani OSMSuspects ya dooley sasa inapatikana kwa watumiaji wote tena. Ukiingia na akaunti yako ya OSM, unaweza kuona metadata.

  • Leif Rasmussen alipendekeza kuongeza ratiba ya usafiri katika OSM katika pendekezo. Kama ilivyovyotarajiwa, watu wengi hawakukubaliana na kuongeza ratiba katika maelezo yao kamili na ya kina.Ni kiasi kikubwa cha data, ambacho hubadilika mara nyingi. Itakuwa daima katika mtindo wa kizamani hivyo vigumu kutegemea.

  • Simon Poole hakubaliani na mazoezi ya sasa ya kugawanya vitambulisho kama languages=<code>;<code>;<code> na language:<code1>=yes + language:<code2>=yes. Anaona kuwa hii inafanya kuwa vigumu kwa watumiaji wa data na waandishi wa mhariri.

Jamii

  • Opencagedata.com imechapisha mahojiano na Russ Garrett wa OpenInfraMap.org. Russ, aliyekutana na Steve Coast katika baa mwaka 2005, anaongoza mradi wa OpenInfraMap.

  • Mshiriki wa kikundi cha kazi cha data mavl, aliripoti katika blogu yake kuhusu ujumbe za kwanza 1000 ambazo zimepokelewa kutoka kwa zana mpya ya kutoa taarifa ya openstreetmap.org. Karibu asilimia 60 ya taarifa hizo zilikuwa zinahusu watumiaji, ikifuatwa na maelezo ya OSM. Bila kujali kitu cha wasiwasi, sababu kuu ya ripoti ilikuwa spam

Taasisi ya OpenStreetMap

  • Frederik Ramm, mshirika wa bodi ya OSMF na mfadhili wa OSMF, aliripoti kuhusu uvumi wa makampuni mawili ambayo hayajajulikana ambayo “yanahamasisha” wafanyakazi wao kujiunga na OSMF,na kuwapa mapendekezo ya uchaguzi na kulipa ada ya uanachama.

  • Rory McCann anaeleza katika orodha ya barua pepe ya OSMF jinsi mwajiri anaweza waambia wafanyakazi wale ambao wanapaswa kupigia kura na jinsi hii inaweza kuthibitishwa licha ya “haijulikani” uchapisho wa kura.

  • Tunajiunga na Michael Reichert na wito wa watu wengine kuwa mwanachama wa OSMF. Mjumbe wa bodi tu anaweza kuhakikisha kwamba bodi ya OSMF itatenda daima kwa maslahi ya watengenezaji wa ramani. Ikiwa unataka kupiga kura katika uchaguzi wa mwaka huu,unapaswa kujiunga kabla ya Novemba 15. Aidha, karibu vikundi vyote vya kazi vya OSMF vinatafuta msaada.

  • OSMF imekuwa ikifanya kazi katika kurekebisha OpenStreetMap API (Rails Port and CGIMap) ili kuzingatia Kanuni ya Ulinzi ya Takwimu Mkuu na imetangaza ombi la zabuni kala ya 15 Novemba.

Matukio

  • Mkutano wa tatu wa State of the Map Czech utafanyika mnamo tarehe 17 hadi 18 mwezi wa Novemba 2018 katika mjii wa Brno.

OSM ya Kibinadamu

  • Shirika la Humanitarian OpenStreetMap Erasmus+ wanafunzi walitangaza katika tweet, kwamba walikuwa wameendesha kozi ya wiki-mrefu inayoitwa kufundisha walimu. Mpango huo ulikuwa na wigo mpana na mada ikiwamo kutengeneza ramani, programu ya Overpass, OSM Wiki, njia za mawasiliano na mengine. Mpango huu umeonyesha uwezekano wa OSM kwa majibu ya kibinadamu na msaada wa maendeleo ya kiuchumi na kupainia viongozi (ambao ni waenye hiari) .

  • HOT inahitaji usaidizi juu ya wiki chache zinazofuata, kutambua idadi ya wakimbizi wa Venezuela walio katika kisiwa cha Aruba.

  • Shirika la Humanitarian OpenStreetMap Team imemaliza kutengeneza ramani ya miundombinu, hasa majengo, barabara, na vipengele vya maji huko Semarang, mji mkuu wa tano wa Indonesia.

Ramani

  • Programu ya Magic Earth Navigation sasa inatumika katika programu ya CarPlay ya Apple baada ya sasisho la hivi karibuni, kulingana na hii ripoti (de) (tafsiri ya moja kwa moja).

  • Nicolas Bétheuil alieleza kuhusu ramani yake ya usafiri wa umma katika orodha ya burua pepe ya Kifaransa . (fr)(tafsiri ya moja kwa moja).

  • Template ya JOSM ya ramani ya Xmas ilirekebishwa na Negreheb kwa taarifa fupi (tafsiri ya moja kwa moja) ana akachapisha katika tovuti ya wiki (tafsiri ya moja kwa moja).

switch2OSM

  • Pristina, mji mkuu wa Kosovo, inatumia ramani ya OpenStreetMap kama ramani yao rasmi ya utalii. Stereo; (Guillaume Rischard) amendika makala kuhusu safari yake huko Kosovo, mkutano na jumuiya ya OSM, na kushawishi Manispaa ya Pristina kutumia ramani ya OpenStreetMap.

Open Data

  • OpenGeoHub imetangaza kutolewa kwa kwanza wa LandGIS, mfumo wa ramani ya wavuti iliyo sawa na OSM, ya data zinazohusika na ardhi na mazingira.Mradi huo inaeneza (au kwa maneno mengine inashindana) na OSM.

  • Statistics Canada imejadili kuhusu Open Database of Buildings, na inashirikiana na jumuiya ili kuagiza katika mikoa tofauti ya Canada.

Programu

  • Simon Poole aliandika kuhusu kutoendelea kwa Google Play ya Android 2.3 and 3.x katika blogu yake na nini inamaanisha kwa Vespucci, ambayo bado inatumia matoleo haya ya Android. Pia anaelezea jinsi ya kutumia Vespucci kwa vifaa ambavyo vina RAM iliyo chini sana

Programming

Vingine vya kijeographia

  • Justin O’Beirne ameandika makala kuhusu uchapishaji wa ramani mpya ya Apple na anaeleza jinsi ramani hizo ni tofauti na za zamani kwa kuonyesha mabadiliko ya kuvutia, kama kiasi cha kina cha mimea. Soma zaidi juu ya swala hili katika blogu yake.

Kumbuka: Ikiwa ungependa kuona tukio lako hapa, tafadhali ongeza tukio hilo kwenye kalenda. Data iliyopo tu ndiyo itaonekana kwenye weeklyOSM. Tafadhali angalia tukio lako katika kalenda yetu ya uma, hakikisha na sahihisha ambapo inafaa.

Discussion

Comment from -karlos- on 4 December 2018 at 11:03

This is not English

Comment from alexkemp on 4 December 2018 at 15:13

First image is broken.

URL=https://www.openstreetmap.org/pristina-osmweekly.png%20=900x900 (gives 404 File not found)

Comment from alexkemp on 4 December 2018 at 15:26

Why on earth are you promoting a blog post for the 1st week of November in December?

Comment from Laura Mugeha on 4 December 2018 at 18:38

These are blogs that had been worked on but could not be posted.

Log in to leave a comment